Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeonyesha kwa vitendo nia yake ya kuinua wakulima wadogo wa makundi maalum nchini kwa kufanya mafunzo ya siku 3 kwa Kituo cha Wakulima Wafugaji Viziwi Tanzania (KIWAWAVITA) yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo kwa nadharia na vitendo wakulima hao ili wainuke kiuchumi, kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo.
Mafunzo hayo yalijumuisha mada kama:
📖 Elimu ya fedha na biashara 👨🌾 Kilimo cha bustani na mbogamboga 🥑 Kilimo cha kisasa