Waziri Nchemba: TADB yaongeza tija katika kilimo kwa mwaka 2022

TADB huongeza tija katika kilimo, kuwezesha utekelezaji wa miradi na kuchagiza ukusanyaji na uuzaji wa mazao ya kilimo kama alivyoeleza Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba, Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango katika uwasilishaji wa bajeti ya wizara hiyo tarehe 8/6/2023, Bungeni, Dodoma.

Katika mada hiyo Dk.Mwigulu aliainisha baadhi ya mambo yaliyowezeshwa na TADB kwa mwaka 2022 kama ifuatavyo:

  • Hadi Desemba 2022, Shilingi bilioni 33.22 zilitolewa kupitia mfumo wa ukopeshaji wa moja kwa moja wa miradi yenye lengo la kuongeza tija katika uzalishaji.
  • TZS 44.2 bilioni zilikopeshwa kwa wakulima wadogo kwa ajili ya miradi ya kuzuia upotevu wa mazao, ambapo TZS. bilioni 35.9 zilitolewa kupitia mfumo wa ukopeshaji wa moja kwa moja na TZS 8.3 bilioni kupitia Mpango wa Udhamini wa Mikopo kwa Wakulima Wadogo (SCGS).
  • Aidha, TZS 97.7 bilioni zilikopeshwa kwa wakulima wadogo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kuwezesha upatikanaji wa masoko ya mazao ambapo TZS 81.3 bilioni zilitolewa kupitia mfumo wa ukopeshaji wa moja kwa moja na TZS 16.4 bilioni zilitolewa kupitia Mpango wa Udhamini wa Mikopo kwa Wakulima Wadogo (SCGS).

Pia, ili kuchagiza uwekezaji katika sekta ya kilimo, benki ilifanikiwa kushawishi benki moja (1) ya biashara kujiunga na Mpango wa Udhamini wa Mikopo kwa Wakulima Wadogo (SCGS).