Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania anaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kufungua milango ya uchumi wa kidiplomasia.
Pamoja na mambo mengine, uchumi wa kidiplomasia katika kilimo unaangazia;
- Kukuza biashara ya mazao ya kilimo kati ya nchi.
- Kuchochea uwekezaji katika kilimo.
- Kuwezesha ushirikiano na taasisi, mashirika na mataifa mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania – TADB, Frank Nyabundege, Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Grace Olotu na Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA, Bi. Jacqueline Mkindi katika mkutano wa uwekezaji wa SWEACC (Sweden East Africa Chamber of Commerce) uliofanyika nchini Sweden, Mei 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania – TADB, Bw. Frank Nyabundege (katikati), Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt Elsie Kanza na afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakifuatilia mkutano kuhusu mipango ya maendeleo na uwekezaji wa sekta binafsi nchini Tanzania.
Mkutano huo uliandaliwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na ulifanyika Washington DC, Marekani mwezi Aprili 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania – TADB, Frank Nyabundege (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt Elsie Kanza akifuatilia mkutano wa mipango ya maendeleo na uwekezaji wa sekta binafsi nchini Tanzania, Washington DC, Marekani.