Bunge liliidhinisha jumla ya TZS 15.9 Trilioni kwa ajili ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2023/2024 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mafungu yake tisa ya bajeti ambapo kwa TZS 15.38 bilioni ni kwa matumizi ya kawaida na TZS 564.22 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw.Frank Nyabundege, akifuatilia Bajeti ya Wizara ya Fedha iliyowasilishwa na Waziri Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba Juni 7, 2023, Bungeni Mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa timu ya Menejimenti ya TADB, wakifuatilia uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2023/2024 Bungeni, Dodoma.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Vihatarishi na Uzingatiaji, Bw.Kassim Bwijo, Mkurugenzi wa Fedha, Dk.Kaanaeli Nnko, Meneja Hazina, Bi.Beatrice Mrema, na Katibu Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Bibi Colletta Ndunguru.