Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiipongeza TADB kwa kazi inayofanya katika sekta ya mifugo
Ameitaka TADB kuendelea kushirikiana na Wizara katika kutengeneza mpango mkakati wa mradi wa vijana katika ufugaji.
TADB kupitia mradi wa Ushirikiano wa Ushirikiano wa Wasindikaji na Wazalishaji Tanzania (TI3P):
- Imetoa mafunzo kwa wafugaji 33,126
- Imeunda vikundi 717 vya wazalishaji wa maziwa
- Kuwezesha vituo 17 vya kukusanyia maziwa vyenye uwezo wa kupokea zaidi ya Lita 29,000 kwa wakati mmoja.
Hadi Desemba 2022 TADB imetoa Shilingi Bilioni 17.7 kwa sekta ya maziwa nchini.
Mhe. Waziri Ulega akikabidhiwa zawadi na wafanyakazi wa TADB katika maadhimisho ya Wiki ya Unywaji wa Maziwa Mkoani Tabora
Wafanyakazi wa TADB wakiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya Wiki ya Unywaji wa Maziwa, Mkoani Tabora