Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhamisi tarehe 6 Julai, 2023 amezindua rasmi Ofisi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Kanda ya Kusini mkoani Mtwara.
Ofisi hiyo iliyopo Raha Leo Complex, Mtwara mjini itahudumia wazalishaji, wasindikaji na wajasiriamali wa minyororo ya thamani ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.
“Napenda kuupongeza Uongozi wa TADB kwa kuanzisha Ofisi hii ya Kanda ambayo itaimarisha huduma za kifedha katika Mikoa ya Kusini na kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, wavuvi na wafugaji kutoka mikoa yote mitatu ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. – alisema Mhe. Majaliwa.