Benki ya Wakulima TADB inaungana na wakulima wote katika kuadhimisha msimu wa wakulima na kusherehekea pamoja jijini Mbeya kuanzia tarehe 1-8 Agosti katika viwanja vya John Mwakangale.
Mkurugenzi Mkuu wa TADB, Frank Nyabundege akipewa maelezo ya Elisante Richard kutoka kwa wanufaika wa Eat Fresh TADB walioonyesha bidhaa zao kwenye Banda la TADB kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa “Nane Nane” John Mwakangale, Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB aliambatana na Ag. Mkurugenzi wa Mikopo na Maendeleo ya Biashara Afia Sigge, Meneja Uhusiano wa Umma na Masoko Amani Nkurlu, Ag. Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti Mkani Waziri na Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mike Granta
Mtumishi wa TADB Angelina Nyansambo Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi na Afisa Mwandamizi wa Wakala Erasto Sonelo wakiwa katika Banda la TADB tayari kwa kupokea na kuwahudumia wageni katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo “Nane Nane” 2023 John Mwakangale gounds, Mbeya.
Mradi wa Ubia wa Wasindikaji na Wazalishaji Shirikishi Tanzania (TI3P) – Mratibu wa Mradi kutoka TADB Joseph Mabula akitoa maelezo kwa wageni na wanufaika wa TADB (Tanzania Delicious Korosho – TDC) kuhusu mradi wa TI3P.
Meneja wa TADB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mike Granta kushoto akizungumza na AnnaMariam Leon wa Kampuni ya Alizeti ya Naki kutoka Manyara katika Banda la TADB, kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo “Nane Nane” 2023 viwanja vya John Mwakangale, Mbeya.
Pia tuliendesha mafunzo kwa wakulima zaidi ya 50 kutoka Igoma AMCOS – Mbeya kuhusu mwenendo wa kilimo biashara, elimu ya fedha na mikopo pamoja na kuongeza uelewa juu ya Miradi ya Udhamini wa Mikopo kwa Wakulima Wadogo (SCGS) na bidhaa na huduma nyingine za TADB.