Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) akitembelea banda la TADB katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo “Nane Nane” 2023, Mbeya.

Mhe. Majaliwa akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti Bw.Mkani Waziri na kuelezwa kuhusu maendeleo ya benki pamoja na taarifa za utoaji wa mikopo, faida, pamoja na idadi ya wanufaika wa mikopo ya benki katika mikopo ya vijana na wanawake.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Majaliwa ameitaja TADB kuwa ni taasisi iliyopewa jukumu la kuleta mabadiliko ya kilimo nchini.

Pia ameiagiza TADB kupanga na kuzishawishi benki na taasisi nyingine za fedha kupunguza riba ya mikopo hiyo kuelekea sekta ya kilimo.

Mhe. Majaliwa pia alipata fursa ya kujionea kazi zinazofanywa na wanufaika wa TADB wakiwemo kahawa ya TANICA (kutoka Kagera) katika sekta ya kahawa, na Kampuni ya JND Polybags (kutoka Iringa), watengenezaji wa kuhifadhi nafaka ambayo inachangia mkakati wa “usimamizi wa mazao baada ya mavuno”.

Mhe. Waziri Mkuu aliongozana na Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Waziri wa Mifugo Mhe. Abdallah Ulega, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde.