Kufuatia mpango mkakati wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania uliozinduliwa hivi karibuni, TADB imeshiriki katika mkutano maalum wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi na wahadhiri kwa mafanikio mbalimbali ya kitaaluma yaliyopatikana mwaka 2023.
TADB ilishiriki na kuwatunuku wanafunzi kumi bora waliohitimu katika mkutano huo ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo.
Tuzo hiyo ni sehemu ya mipango ya TADB ya kuendeleza ushirikiano wa kimkakati kati ya TADB na SUA. Pia, inaunga mkono mipango ya serikali katika kufikia #Ajenda 10/30 ambapo #vijana wana jukumu muhimu la kuimarisha hilo.
TADB itaendelea kushirikiana na SUA katika kuboresha mazingira ya vijana, kujifunza kwa kufanya na kuwajengea uwezo ili kuongeza ubunifu na kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya kilimo.
TADB tunaamini kuwa kuwekeza kwa vijana ni muhimu kwa maendeleo endelevu na kesho yenye mafanikio💪🏾