Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) ameipongeza TADB kwa kazi nzuri, na kusisitiza juhudi zaidi katika kuboresha sekta ya kilimo.
Waziri Mkuu Majaliwa ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa mchango wake wa kutoa mikopo yenye riba nafuu na hivyo kusaidia kuboresha maisha ya wakulima na uchumi wa nchi ambao kwa kiasi kikubwa unategemea kilimo.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatano Novemba 22 wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma za Kifedha jijini Arusha.
Alisema, Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na benki hiyo katika kuleta mageuzi katika kilimo kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima wa Tanzania na kutaka iendelee.