ARCHIVE ya Ukurasa

TADB inaahidi kuimarisha ufadhili wa sekta ya mifugo

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema itaendelea kufadhili sekta ya mifugo ili kuwezesha sekta hiyo kuongeza mchango katika uchumi. Hayo yamesemwa na afisa maendeleo ya biashara mwandamizi wa benki hiyo Furaha Sichula wakati wa maonyesho na mnada wa kwanza wa mifugo uliofanyika Ubena Zomozi wilayani Chalinze mkoani Pwani.